Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Zainab Abdallah amewataka Wakandarasi wanatekeleza miradi ya maendeleo Wilayani humo kukamilisha miradi hiyo kwa wakati kwani kuwa na miradi mingi hupelekea miradi hiyo kuta kukamilika kwa wakati na hivyo kupelekea sintofahamu kwa wananchi juu ya miradi hiyo.
Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo Wilayani humo katika kikao kazi na Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya taasisi zote za Serikali kuu.
Akizungumza kwanjia ya simu na mkandarasi aliefahamika kwa jina la Kareem ambaye anatekeleza mradi wa maji wilaya huyo Dc zainab amemtaka mkandarasi huyo kumaliza mradi huo kwa haraka ifikapo mwezi wa tano mwaka huu na sio vinginevyo.
“Yani kwakweli Karibu siwezi kukuelewa kwasababu mradi ulitakiwa ukanilike mwezi wa tatu wewe ukaomba hadi mwezi wa Tano na hadi sasa bado kwanini nyie wakandarasi mnatabi ya kuwa na miradi mingi sehemu mbalimbali sasa ukiona pangani hatukusumbui unachukua fedha za pangani unapeleka sehemu nyengine huku tuna kwama hii haikubaliki na fika unafahamu hili ni jimbo la waziri wa Maji labda kama unataka usipate miradi mingine ya Maji sawa”- Alisema DC
DC Zainab mesema kuwa Mhe.Rais amekuwa akileta fedha nyingi kwaajili miradi mbalimbali ya maendeleo kwa Wananchi hivyo kama viongozi ambao wapo chini ya Mhe.Rais hata kubali dhamira ya njema alio nayo kwa wananchi wake isifikiwe na wazembe wachache.