Halmashauri ya wilaya ya Kwimba ni moja ya Wilaya Kongwe zinazopatikana mkoani wa Mwanza, wilaya hii inakadiriwa kuwa na watu zaidi ya 500,000, kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, upekee wa wilaya hii ni kuwa hajapitiwa na ziwa Victoria licha ya kuwa ipo Kanda ya ziwa pamoja na kuwa shughuli kuu za wakazi wa eno hili ni kilimo na ufugaji lakini biashara zingine zinaendelea, kutoka Barabara Kuu ya Mwanza, Shinyanga ni umbali wa kilometa zisizopungua 30, kufika Ngudu makao makuu ya wilaya ya Kwimba.
Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri ya kwimba ilikusanya mapato kiasi Tsh. Billioni 2.6, huku 2022/2023 imekusanya kiasi cha fedha Tsh. Billioni 3.43, na kiasi cha fedha zaidi ya Billioni moja zimepelekwa kwenye miradi ya maendeleo ambapo Wananchi wamenufaika nayo moja kwa moja
Ngwi’labuzu Ludigija yeye ni Mkuu wa wilaya wa 29, katika orodha ya wakuu wa wilaya waliowahi kuhudumu wilaya Kwimba, ameeleza miradi ya kimaendeleo iliyofanyika ndani ya miaka miwili chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye awamu ya sita.
Pamoja na mengine Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kwimba Happiness Msanga amefafanua utekelezaji wa miradi na shughuli za kimaendeleo ikiwemo utoaji wa huduma za kijamii kupitia mapato yake ya ndani, huku akibainisha jitihada za Serikali zilizofanyika kufikisha huduma kwa Wananchi wa Kwimba katika sekta ya Afya na Elimu.
Ayo TV, millardayo.com imefanya mahojiano maalum katika video hii, unaweza kutazama kwa undani.