Jeshi la Polisi limesema limeona video fupi (clip) ikimwonesha Mtoto aliyefanyiwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji na limeanza kuifanyia kazi kuanzia ilipoanza kusambaa ili aliyefanya kitendo hicho cha kinyama kisichokubalika aweze kukamatwa na hatua nyingine za kisheria ziweze kufuata.
“Mtoto huyu lazima atakuwa na Mama, Babu, Bibi, Shangazi, Mjomba, Majirani na Viongozi wa Serikali za Mitaa, tunatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za nani alifaya kitendo hicho au kilifanyikia wapi asisite kutoa taarifa Polisi au kwa Kiongozi yeyote yule ili kufanikisha kukamatwa kwake”