Wakati idadi ya watalii wa kimataifa ambao hufika nchini Tanzania kwa shughuli za kitalii na mapumziko ya mwaka, ikitabiliwa kushuka kutokana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa COVID-19 Duniani kote, Shirika la hifadhi za taifa nchini TANAPA, tayari limo katika hatua za mwisho za kukamilisha mradi maalumu kwa ajili ya watalii wa ndani,wa kutizama wanayama adimu aina ya faru kwa karibu.
Akiwa katika hifadhi ya taifa ya Mkomazi wilayani same mkoani Kilimanjaro baada ya kukagua baadhi ya Miundombinu muhimu ya mradi huo huo, katibu mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii prof Adolf Mkenda amesema, mradi huo ni fursa mpya kwa utalii wa ndani pamoja na pato la Taifa hasa kipindi hiki cha corona.
Kwa upande wake Mwandamizi kanda ya kaskazini kutoka shirika la hifadhi za taifa nchini Tanapa, Helman Beteho anaeleza hatua ambazo zimefikiwa katika ujenzi wa mradi huo, mkuu wa Wilaya ya same bi Rosemery Senyamule akatoa wito kwa watanzania kutumia fursa ya kuwepo kwa mradi huo ambao utaongeza mapato ya TANAPA na taifa kwa ujumla.
VIDEO: BAADA YA LIGUE 1 NA LIGI KUU KENYA KUFUTWA, NIYONZIMA ANAUSHAURI HUU VPL