AyoTV

VIDEO: Kaseja hili ndio jibu lake wanaouliza atastaafu lini? “Nacheka, nakukebehi tu!”

on

Leo AyoTV imefanya exclusive interview na golikipa wa zamani wa Simba SC, Yanga SC ambaye kwa sasa anaichezea KMC ya Kinondoni Juma Kaseja aliyepewa jina la Tanzania One kutokana na umahiri wake wa kudaka hususani mikwaju ya penati.

Kaseja yupo kwenye game kwa muda mrefu toka mwanzoni mwa miaka ya 2000 akiichezea Moro United na amefanya makubwa sana ngazi ya club na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, kumekuwepo na maneno mengi kuhusiana na Kaseja.

Wengine wanasema kuhusiana na Kaseja atastaafu lini sababu amecheza kwa muda mrefu? Kaseja ameongea kupitia AyoTV kuwa watu ambao huwa wanamuuliza maswali hao huwa anawacheka na kuwapuuzia na kuwaweka katika kundi lao sababu haoni umuhimu wa kupewa presha ya kustaafu wakati ana uwezo wa kucheza.

AUDIO: SIMBA SC ILIVYOMPOKEA MEDDIE KAGERE LEO

Soma na hizi

Tupia Comments