Kocha wa Tanzania bara Juma Mgunda baada ya kurejea Tanzania akitokea Uganda katika michuano ya CECAFA timu yake ikiishia nafasi ya nne ameeleza sababu za kikosi chake kufanya vibaya katika michuano hiyo tofauti na matarajio ya watanzania walio wengi.
“Tumecheza michezo mitano ya kimataifa sio rahisi kuipata kama timu ya taifa, kwa hiyo hata wale vijana tuliokwenda nao kwa nilivyowaona nyinyi wenyewe mtakuwa mashahidi, hatukufanya vizuri lakini hatukufanya vibaya sana katika timu angalau tumekuwa wanne, mashindano yalikuwa mazuri lakini yalikuwa magumu kila baada ya saa 48 tunacheza”>>>Mgunda
AUDIO:BREAKING: NIYONZIMA KARUDI YANGA SC