AyoTV

VIDEO: Kocha Mkwasa afunguka “Waliosajiliwa na Zahera wakijipanga nitawapa nafasi

on

Baada ya ushindi wa Yanga wa goli 1-0 lililofungwa na Patrick Sibomana dakika ya 75 ya mchezo dhidi ya Ndanda FC, kaimu kocha mkuu wa Yanga SC Charles Boniface Mkwasa aliongea na waandishi wa habari.

“Mechi imekuwa ngumu sana lakini vijana wamejitahidi sana, tumetengeneza nafasi nyingi lakini tumezikosea kwa sababu ndio tunaanza, nimefanya training kama siku moja tu, tunaangalia yale makosa muhimu ambayo tunaweza kuyarekebisha”>>>Mkwasa

“Wachezaji wa Yanga wote ni wazuri walisajiliwa wengine hawajapata nafasi ya kucheza, naamini yoyote ambaye amesajiliwa ni mchezaji mzuri na akiwa amejiandaa vizuri nitampa nafasi ya kucheza”>>>Mkwasa

VIDEO: BAADA YA KUFUKUZWA AYO TV IMEMFUATA ZAHERA KWAKE “SIJAPEWA BARUA”

Soma na hizi

Tupia Comments