AyoTV

VIDEO: Kocha Mpya Yanga katua Dar, kajibu ishu za kutodumu na timu

on

Kocha Mkuu wa Yanga SC raia wa Ubelgiji Luc Eymael amewasili leo Dar es Salaam Tanzania na kuunganisha ndege moja kwa moja kuelekea Zanzibar ilipokuwa timu katika michuano ya Mapinduzi Cup kwenda kuangalia mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Yanga SC dhidi ya Mtibwa Sugar leo.

Luc mwenye umri wa miaka 60 amewasili na kuweka wazi majibu kuwa huwa hadumu na timu na mara nyingi huwa anadumu na timu kwa kipindi cha mwaka mmoja au miezi sita, Mr Luc amejibu kuwa sio kweli amekaa na timu nyingi tu muda mrefu ikiwemo alipokuwa Gabon.

“Sio mara yangu ya kwanza kuja Tanzania niliwahi kuja na Vita Club nina furahi kuwa hapa katika timu kubwa kama Yanga na nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuipandisha kiwango zaidi Yanga na kuirudisha katika hali yake ya ushindi”>>>Luc Eymael

VIDEO: KUMLAUMU AISHI MANULA NI KUMKOSEA HESHIMA BALAMA WA YANGA

Soma na hizi

Tupia Comments