AyoTV

VIDEO: Kocha wa Yanga aeleza alivyoangushwa na Yikpe na Molinga uwanja wa Taifa

on

Cluba ya Yanga SC katika mchezo wake wa Ligi Kuu uliyochezwa uwanja wa Taifa dhidi ya Lipuli FC na Yanga kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ambayo yalifungwa na Mapinduzi Balama dakika ya 14 na Bernard Morrison dakika ya 31 kwa upande wa Yanga huku la Lipuli FC likifungwa na Mwassa dakika ya 58.

Kocha mkuu wa Yanga SC raia wa Ubelgiji Luc Eymael amefunguka mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na kuhuzunishwa na kiwango cha timu yake hususani kipindi cha pili, Luc ameeleza pia kuwa washambuliaji wake tegemeo wawili David Molinga na Yikpe wamemuangusha katika mchezo dhidi ya Lipuli FC.

VIDEO: KIPATO HULETA MAJIVUNO, ANTONIO NUGAZ WA YANGA ANATAMBA TU!!!

Soma na hizi

Tupia Comments