Top Stories

VIDEO: Kutoka Zanzibar Mtoto Said Ally ameanza matibabu

on

AyoTV na millardayo.com zimefika mpaka hospitali ya Mnazi Mmoja inayopatikana Zanzibar mahali ambapo amelazwa mtoto Said Ally ambaye anasumbuliwa na tatizo la Kansa.

Tumezungumza na Bwana Rashid Mohamed ambaye ni msemaji wa familia na ndiye mtu aliyewasaidia kuonesha tatizo la mtoto huyo kwa Mara ya kwanza yeye amesema

“Siku ya jumatatu tulianza pilika ya kumsafirisha mtoto, lakini mashirika ya ndege yalipojua hali ya mtoto wakakataa kumsafirisha, wakatuelekeza tupate barua ya Daktari itakayoweza kuthibitisha mtoto kusafiri na kama hata kuwa na athari kwa watu wengine,

nilipigiwa simu na watu wengi kwamba Makonda anakutafuta, nilizungumza naye na aliniambia anamtaka mtoto Leo alale Daresalaam na Tayari madkatari wapo na Ambulance yakumchukua airpot ipo, nikampigia waziri wetu ambaye alisema tukutane na tukaelekea Mnazi Mmoja ambapo mtoto akapewa kitanda” – Rashid ( Msemaji )

Pia Rashid ameelezea michango waliyofanikiwa kuikusanya mpaka sasa kufikia milioni 7 na zote wameziweka kwenye utaratibu mzuri wa kuhakikisha zinamsaidia kwenye matibabu mtoto huyo.

Mpaka jioni ya February 19, 2019 mtoto Said alikuwa hospitali ya Mnazi Mmoja licha ya kuwa watu mbali mbali wamejitokeza kutaka kumsaidia wengine wakitaka apelekwe Muhimbili, Au KCMC Moshi.

Full story ya hii ipo hapa chini Bonyeza PLAY kutazama VIDEO

Soma na hizi

Tupia Comments