Top Stories

VIDEO: Majirani washindwa kuzungumza kisa mfereji wa maji

on

Baada ya mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo nchini wananchi wa mtaa wa Pwani kata ya Kunduchi katika manispaa ya Kinondoni nao wamekumbwa na kadhia hiyo ya mafuriko.

Mafuriko hayo yameleta hali ya kutokusalimiana kwa majirani hao zaidi ya kumi na moja baada ya majirani wa upande mmoja kuomba kibali TARURA cha kuchimba mfereji ambao utaruhusu maji kupita na kutoa adha ya maji kujaa katika maeneo yao makazi huku upande mwingine wa majirani hao wakikataa mfereji huo kupita kwao wakidai umasababisha mawasiliano ya barabara kukatika kwani wamechimba katikati ya barabara hali inayopelekea akipata mgonjwa inakuangumu kupeleka mgonjwa hospital.

Hali hiyo imesababisha Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta na Meneja wa TARURA wilaya hiyo Leopold Runji kufika eneo hilo na kutoa maamuzi ua kumaliza ugomvi huo ambao umedumu kwa mda mrefu hali iliyopelekea mpaka kupelekana mahakamani kwa majirani hao wa mtaa mmoja

Bonyeza PLAY kutazama VIDEO

Soma na hizi

Tupia Comments