Mix

VIDEO: Mambo manne ya kuepuka unapotaka kuandaa harusi yako

on

Kama una mpango au jamaa/rafiki ana mpango wa kufanya harusi kwa siku za usoni hii ni elimu imetolewa kupitia TBC 1 ili kuweza kufanya sherehe ya harusi huku ukiwa umekwepa madeni, inadaiwa kuwa maharusi wengi baada ya sherehe uangukia katika adha ya kulipa madeni, basi haya ndio mambo manne ya kuzingatia kama una mpango wa kufanya harusi.

1. Nuia vitu ambavyo vinaendana na uwezo wao.

2. Angalia watu wanaokuzunguka, ndugu, jamaa na marafiki, je! Wanaweza kukusaidia kufanikisha kile ambacho unakitaka bila kuwawekea mzigo mkubwa?

3. Angalia ni kwa namna gani utamaliza shughuli unayoikusudia. Utamaliza ukiwa na madeni, au bila madeni?

4.Angalia kama kuna umuhimu wa vile unavyovifanya, tuweka zulia ukumbi mzima, kuwa na vyakula vingi vya aina moja (wali mweupe, pilau, biriani). Katika maandalizi ya sherehe yoyote ikumbukwe kuwa kuna vitu vya lazima kuwepo, na vingine si vya lazima, lakini unaweza ukawa navyo. Kama si cha lazima, na ukikiweka itatoka nje ya bajeti yako, achana nacho.

VIDEO: MADENI YA HARUSI YANAVYOATHIRI NDOA CHANGA

Soma na hizi

Tupia Comments