AyoTV

VIDEO: Mashabiki wakihoji kiwango cha timu, kocha wa Simba kazungumzia kiwango

on

Baada ya mchezo wa Simba SC kumalizika kwa Simba SC kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania, magoli ya Simba SC yakifungwa na John Bocco dakika ya 57 na Ibrahim Ajib dakika za nyongeza wakati goli la Polisi likifungwa na  Sixtus Sibalo dakika ya 23 ya mchezo.

Utata uliopo kwenye mchezo huo ni goli la kwanza la Simba kudaiwa kuwa Bocco alikuwa offside lakini cha pili ni watu kutokuridhika na uwezo wa Simba SC licha ya kupata ushindi katika michezo kadhaa ya hivi karibuni kiasi cha wengi kuona kocha wao kama sio chaguo sahihi, baada ya game kocha wa Simba SC Sven Vanderbroeck aliongea na waandishi wa habari.

“Nafikiri tulijiwekea maisha magumu wakati wa kipindi cha kwanza na hatukucheza katika kiwango ambacho tulikitarajia, nafikiri kipindi cha pili tulijipanga japokuwa tuliwapa wapinzani nafasi nyingi za kucheza lakini ni vizuri kutengeneza kitu”>>> Sven Vanderbroeck

VIDEO: PAMBANO LA ROUND 10: MTANZANIA VS MTHAILAND NI UBINGWA WA DUNIA

Soma na hizi

Tupia Comments