Ni Desemba 11, 2022 ambapo Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Dkt. Kedmon Elisha Mapana amewaanga rasmi Mpoto Theatre kuelekea katika Tamasha kubwa ambalo litafanyika nchini India.
Lengo la Tamasha hilo ni kuadhimisha miaka 100 ya aliyekuwa Rais Pramukh Swami Maharaj.
Akizungumza na waandishi wa Habari Katibu Mtendaji wa BASATA alisema..’ Hongereni sana Mpoto na timu yako kwa kupata nafasi hii ya kipekee ya kwenda nchini India Kutumbuiza ni fursa kwa wasanii wetu na mimi nawakabidhi kibali hiki rasmi cha kuwaruhusu muende ukaoneshe yale mliyonayo na mkaitangaze Tanzania vyema”– Dkt. Kedmon Elisha Mapana
‘Niwatakie kila la heri basi muwakilishe vizuri, vijana wetu ni bado wadogo wapige kazi ya sanaaa na ndivyo Mheshimiwa dkt Rais Samia anapenda wasanii amewapa nafasi nzuri na tunasema katika awamu ya sita sanaa imepewa kipaumbele sana tuendelee kuchapa kazi kwelikweli’- Dkt. Kedmon Elisha Mapana
Aidha Mrisho Mpoto alizungumza na waandishi wa habari juu ya Tamasha hilo na kusema..‘Tuko hapa kwaajili ya kuwaaga Mpoto Theatre imepata baraka na bahati kubwa ya kushiriki kwenye Tamasha kubwa litakalofanyika pale India ambalo Tamasha litachukulia siku zisizopungua 30 mpaka 40″
“Tamasha hili linaitwa PRAMUKH SWAMI MAHARAJ ni tamasha ambalo wanasheherekea muasisi wao ambae anatimiza miaka 100 kwahiyo wahindi wote na madhehebu yote wanakutana pale India kusheherekea katika mwezi huu wa kumi na mbili mpaka mwezi wa kwanza”- Mrisho Mpoto
“Tunasubiriwa kwa hamu sana na kingine nisipotoa shukrani kwa pekee kwa Mheshimiwa Rais kupitia Royal Tour basi Mpoto Theatre isingejulikana hivyo ni fursa ya kipekee kabisa lakini pia Mpoto Theatre ina models lengo kutambulisha mavazi na sanaa yetu izidi kuwa kubwa zaidi na zaidi”