AyoTV

VIDEO: Musonye anaua CECAFA? hili ndio jibu lake

on

Kumekuwepo na tetesi mbalimbali kuhusiana na kile kinachodaiwa ni kudhorota kwa mashindano mbalimbali yanayoandaliwa na CECAFA, kila mmoja amekuwa akitoa mawazo yake na wengine kukinzana ila jibu la CECAFA inakwama wapi bado halijapata jibu.

Baadhi ya watu wamewahi kumtuhumu chini kwa chini kuwa katibu mkuu wa baraza la vyama vya soka na vilabu vya Afrika Mashariki maarufu kwa jina la CECAFA, Nicolaos Musonye ndio tatizo na anapelekea baraza hilo kufa, Musonye ametoa jibu leo akiwa Lugogo jijini Kampala nchini Uganda katika mkutano mkuu wa CECAFA.

“Umeona huu mwaka pekeake tumeandaa mashindano sita nchi nyingine gani ambayo inaweza kuandaa mashindano kama haya, watu nyine mnasema Musonye anaua CECAFA mimi ndio nimeshika hii kitu miaka yote ningeua nyine mngekuwa hapa? mimi nasema tumeandaa mashindano yetu na kuona CECAFA imesimama imara”>>> Musonye

AUDIO: HARUNA NIYONZIMA ANARUDI YANGA? BUMBULI KATOA JIBU

Soma na hizi

Tupia Comments