Leo imeripotiwa kuwa Rais wa shirikisho la soka Tanzania Wallace Karia ameagiza kuwa kamati ya waamuzi na bodi ya usimamizi na uendeshaji wa Ligi Bodi ya Ligi (TPLB) kukutana na kujadili mambo mbalimbali hususani kuhusiana na viwango vya waamuzi kudaiwa kuporomoka katika baadhi ya michezo ya Ligi Kuu.
Kwenye mechi tatu sasa mashabiki na baadhi ya timu wamekuwa wakidai kuwa Simba SC inapendelewa na waamuzi, huku wengine wakidai ni maamuzi mabovu tu ya waamuzi, kuna mechi Kagere wa Simba alifunga goli linalodaiwa kuwa off side muwamuzi akakubali na kuna mechi nyingine Kagere alifunga goli linalodaiwa kuwa halali refa akakataa akasema offside.
Jana Simba SC goli la kusawazisha la Simba SC dhidi ya Polisi Tanzania katika ushindi wa Simba wa 2-1, goli likifungwa na Bocco dakika ya 57 inadaiwa kuwa ilikuwa offside refa akakubali, leo tunae katika exclusive interview muigizaji Ray Kigosi ambaye pia ni shabiki wa Yanga kwa upande wake yeye akiongea kama mdau wa soka anaonaje kiwango cha waamuzi.
VIDEO: KOCHA WA YANGA AELEZA ALIVYOANGUSHWA NA YIKPE NA MOLINGA TAIFA