Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema ameona taarifa kuhusu baadhi ya Watu kuwa na adhima ya kuandamana Jijini Dar es salaam leo wakidai kupinga kilichoamuliwa kuhusu ubia wa uendelezaji wa Bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai ambapo amewataka waliokusudia kuandamana waache mara moja kwa kile alichosema kuwa huu sio muda wa maandamano.
“Ndugu Waandishi wa Habari tumeitana leo Jumatatu ili tuweze kuzungumza baadhi ya mambo ambayo nimeona yameanza kupigiwa kelele kupitia mitandaoni na kupitia kwenye makundi ambao hawalitakii mema Taifa letu”