AyoTV

VIDEO: Samatta baada ya kuwasili pamoja na Msuva DSM

on

Mbwana Samatta baada ya kutua Airport DSM akitokea Ubelgiji, waandishi walimuuliza kuhusiana na timu na taifa la Equatorial Guinea ambayo wanacheza nayo November 15 2019 uwanja wa Taifa game ya kuwania kufuzu AFCON 2021 na November 19 2019 dhidi ya Libya.

“Mimi sijui chochote kuhusu Equatorial Guinea kabisa yaani wala simjui mchezaji hata mmoja kutoka Equatorial Guinea, kwa hiyo siwezi kuwazungumzia wao wala nchi yao sijui ina aina fulani ya watu, nafikiri Tanzania tutakuwa tumeandaa kikosi chetu na tumejiandaa vizuri ili yasije kutokea kama yaliyotoke mwaka juzi (Lesotho)”>>>Samatta

Samatta ambaye amemaliza kuitumia KRC Genk katika mchezo dhidi ya KAA Gent Jumapili ya November 10 2019, amewasili Tanzania alfajiri ya November 12 akiambatana na mshambuliaji mwenzake wa Taifa Stars Simon Msuva akitokea Difaa El Jadid ya Morocco.

VIDEO: JIBU LA SAMATTA KUHUSIANA NA ISHU YA WEST HAM NA NEWCASTLE

Soma na hizi

Tupia Comments