Habari za Mastaa

VIDEO: Shetta akitoka kulikomboa Gari lake, Kafunguka kutumia Milioni 100 toka alinunue

on

Msanii wa Bongofleva Shetta amefanikiwa kulirudisha mikononi kwa kulipia gari lake (Land Rover Discovery) faini ya MILIONI 12.9 baada ya kukamatwa na TRA amesema imemsaidia kuwafahamu Wanafiki na kazi iliyobaki ni kuwapunguza.

Shetta amefunguka kuwa Gari hilo limeshatumia hela zake nyingi toka alinunue ambazo akikadiria zinafika Milioni hata 100, pia ameongezea kwa kusema swala hilo limemfunza kuhusu kulipa kodi na kuwasihi wengine wasikwepe kodi kwani mkono wa serikali ni mrefu utawafikia popote.

Pia hajaacha kuwatumia salamu wasanii waliokuwa wakimcheka baada ya Gari lake kukamatwa maeneo ya Mikocheni DSM na Askari na Maofisa wa TRA kwa kosa la mwaka juzi lililofanywa na aliemuuzia kuzidisha muda wa kutembelea namba za kigeni (za South Africa) kulikomfanya apigwe faini ya MILIONI 12.9

Bonyeza PLAY kutazama FULL INTERVIEW 

Soma na hizi

Tupia Comments