AyoTV

VIDEO: Tathmini ya Zahera game ya Simba na Yanga, kataja wachezaji tishio

on

Kocha wa zamani wa Yanga SC Mwinyi Zahera amefunguka na kueleza tathmini yake ya mchezo wa Simba na Yanga unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumamosi ya January 4 2020, Zahera amesema katika mchezo huo haipi nafasi timu yoyote kwani michezo yake iliyopita kwa timu hizo zote zimeshinda

“Kuhusu Simba na Yanga hakuna timu yoyote ya kusema kwamba naipatia nafasi kwambii hii ndio itashinda nadhani ipo 50% kwa 50%, sababu ukiangalia mechi walizocheza Simba na Yanga mechi mbili za mwisho walishinda wote kabla ya kukutana hiko ni kitu kinachowapati wachezaji morali na kujiamini ndio maana nasema 50% kwa 50%”

“Simba au Yanga hakuna atakayeingia uwanjani na woga wa kusema kwamba hatuko vizuri itakuwaje wote wawili wako vizuri, mechi kama hii ni kubwa ila concetration ikiwa kubwa sana huwezi kuingia kama unacheza mechi ya Ndanda, KMC na Lipuli unaweza fanya makosa mawili matatu na wasikufunge lakini hii mechi ukikosa nidhamu wanakuadhibu”

VIDEO: NIYONZIMA KAWASILI DAR, KAULI YAKE KUHUSU GAME YA SIMBA NA YANGA NDIO HII

Soma na hizi

Tupia Comments