AyoTV

Video ya kwanza ya Hussein Machozi toka afumaniwe na mke wa Mwanasiasa Kenya

on

Screen Shot 2014-08-06 at 12.26.38 PMSiku zinahesabika toka zitoke stori zake Hussein Machozi kuhusu kufumaniwa na mke wa Mwanasiasa maarufu huko Mombasa Kenya ambapo gazeti la Majira Tanzania liliandika msanii huyu Mtanzania amepewa saa 24 kuondoka nchini Kenya baada ya hilo tukio.

Ikiwa bado tunasubiri kusikia kutoka kwake, Hussein Machozi ambae bado yuko Kenya ameitumia millardayo.com hii video yake mpya, ukishaitazama usiache kuandika comment yako hapa chini kwa jinsi ulivyouona wimbo wenyewe na video alafu baadae jioni Hussein atapita hapa kusoma ulichomwandikia mtu wangu.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook kama ukijiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta FB

Tupia Comments