Habari za Mastaa

Video ya Mwisho ya Maunda Zorro muda mfupi kabla ya kifo ‘Aliimba na kufurahi’

on

Msanii wa Bongofleva, Maunda Zorro amefariki dunia kwa ajali ya gari usiku wa kuamkia leo, Kaka wa marehemu ambaye pia ni Msanii wa Bongofleva Banana Zorro ameithibitishia Ayo TV taarifa hizi na kusema hadi jana jioni alikuwa pamoja na Maunda kwenye msiba wa Rafiki yao lakini baadaye akapata taarifa kuwa Maunda amefariki.

“Nimezipata hizo taarifa ndio naelekea Hospitali ya Kigamboni, taarifa ni za kweli tulikuwepo kwenye msiba jioni ya leo wa rafiki yetu mwingine wa karibu, nilikuwa nae Maunda hadi jioni saa 11 hadi 12 nikarudi nyumbani kulala maana msiba ulikuwa Kigamboni na yeye anakaa Tuangoma, kwa taarifa zaidi (kuhusu msiba) ni hadi nikifika Hospitali”

Hapa nimekusogezea ushuhudie video hii ya mwisho ya Maunda Zorro muda mfupi kabla ya kifo ‘Aliimba na kufurahi’

BREAKING: MAUNDA ZORRO AFARIKI DUNIA “ALITOKA MSIBANI”

 

Tupia Comments