AyoTV

VIDEO: Yanga SC yalia ukata yaweka wazi inadaiwa zaidi ya Tsh Bilioni 1

on

Mwenyekiti wa Yanga SC DR Mshindo Msolla leo ameweka wazi kuwa Yanga SC haijawalipa wachezaji wake kwa kipindi cha miezi miwili na ifikapo jioni ya leo basi Yanga watahakikisha wanalipa mishahara ya wachezaji hao kubwa lililopelekea hilo ni kutokana na Yanga SC kuyumba kiuchumi na kuwa na madeni.

DR Msolla pia ameweka wazi kuwa wameingia Yanga SC ikiwa na madeni makubwa sana ambayo hawaweza kuyakwepa, kwani TFF inaidai Yanga SC  zaidi ya Tsh milioni 800, wakati makocha wao wa zamani kama George Lwandamina na Hans van Pluijm kila mmoja akiwa anadaiwa zaidi ya Tsh milioni 100.

VIDEO: PAMBANO LA ROUND 10: MWAKINYO VS TINAMPAY

Soma na hizi

Tupia Comments