Top Stories

VIDEO:DC awafungia biashara SIDO kwa kutovaa barakoa kwa siku tatu

on

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga amewafungia wanaofanya biashara ya mbao kwa siku 3 bila kufanya kazi pamoja na mafundi wa SIDO katika Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa kukiuka agizo alilolitoa mwezi mmoja uliopita kwa kuwataka kuwa na ndoo za kunawia na kuvaa barakoa kwa muda wote wanapokua kazini kwa sababu ni sehemu ya mikusanyiko kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa Covid 19.

Mkuu wa Wilaya amesema watafunga biashara kuanzia tarehe 16 Mei mpaka tarehe 19/05/2020 siku ya Jumanne kwaajili waende kwao kutafuta barakoa.

Soma na hizi

Tupia Comments