Ni Headlines za Harusi ambayo ilitumia zaidi ya bajeti ya Milioni 100 halafu unaambiwa mwisho wa siku ikadumu ndani ya miezi miwili tu, sasa Ayo TV imempata MC Gara B ambae alihusika kusheheresha Harusi hiyo iliyofanyika mwaka 2018 kwenye ukumbi wa uliopo Mlimani City Dar es Salaam.
‘Nakumbuka Harusi hiyo ilifanyika Mwaka 2018 na ndoa hiyo ilikuwa ya miezi miwili na kimsingi inavyoonekana upande wa mke walizingua hivi, sitaki kuzungumzia sana lakini ninachofahamu kwamba Bwana Harusi alipambana sana na ndoa ilikuwa ya zaidi ya Milioni 100 ndio ilikuwa bajeti yao’– Mc Gara B
‘Yule Mwanamke yuko Nchini nyingine na Jamaa hataki kabisa kusikia masuala ya Ndoa mpaka leo yaani akinipigia simu na kuniambia Gara B sitaki masuala ya Ndoa’- MC GARA B