Ni msanii wa Bongo Fleva Alikiba mwenye umri wa miaka 32 ambae headlines zake zilianza mwaka 2005 ambapo kupitia wimbo wa msanii Abby Skillz alijulikana baada ya kushirikishwa katika wimbo uitwao Maria
Safari ya Alikiba ikamuendelea murua ambapo mwaka 2007 aliachia rasmi album yake ya kwanza yenye jina la ‘Cinderella’ yenye nyimbo 15 ambazo zilizopendwa na kukubali.
Ilipofika mwaka 2010 Alikiba alipata shavu kubwa la kuwa miongoni mwa wasanii walioshiriki kuimba wimbo wa Hands Across the World uliyosimamiwa na Staa R Kelly na kusambazwa na Sony Music & Rockstar4000.
Hands Across the World ni wimbo uliokutanisha wasanii 8 kutoka mataifa tofauti Afrika akiwemo, R.Kelly, 2Face, 4×4, Alikiba, Amani, Fally Ipupa, JK, Movaizhaleine & Navio
Ukimya wa Alikiba ulianza mwaka 2010 ambapo mkali huyo aliamua kukaa kimya takribani miaka 4 na aliporudi mwaka 2014 kwenye muziki wa Bongo Fleva aliachia video ya wimbo wake mpya uitwao MWANA.
MWANA ulikuwa ni wimbo wa kwanza uliosimamiwa na lebo ya Rockstar4000 enzi hizo chini ya meneja Seven Mosha, baada ya hapo zikafuata mwendelezo wa hits mbalimbali kali zikiwemo, Seduce Me, Aje, Lupela, Chekecha Cheketua, Kadogo, Mvumo wa Radi na nyinginezo kali
Safari yake ya muziki ikaendelea na ilipofika mwaka 2016 staa huyo alisainiwa na Sony Music ambapo mnamo tarehe 19 mwezi mei Alikiba alifika nchini Afrika Kusini katika ofisi za Sony Music kusainiwa rasmi.
Moja ya kazi za mkataba huo ni kumtengeneza Alikiba kwenye kiwango cha juu zaidi kimuziki, kibiashara na kugharamia video zake na anaporekodi audio zake, kila anapotoa muziki mpya unaachiwa kwa nguvu ya usimamizi wa Sony Music kwenye masoko makubwa ya muziki kama Marekani, Ulaya na Africa.
Unaambiwa mkataba aliokuwa ameusaini Alikiba unafanana na ule aliosaini mwimbaji staa wa Nigeria Davido ambapo una vipengele vya kusababisha collabo kwa urahisi zaidi na mastaa wakubwa wakiwemo wa marekani.
Baada ya kusainiwa na Sony Music tukazishuhudia hits kali na collabo mbalimbali zilizochukua vichwa vya habari
Safari ya Alikiba ikaendelea kupamba moto kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva ambapo mwaka 2018 aliamua kuwatambulisha rasmi wasanii wake anaowasimamia katika lebo yake iitwayo King Music Records
Wasanii hao ni Cheed, K2ga, Killy ambapo single yao ya kwanza ilitambulika kwa jina la Mwambia SINA, Baada ya hapo zikafuata mfululizo wa hits mbalimbali ikiwemo Rhumba, Toto
Kwasasa Alikiba anazimiliki spika za radio kwa wimbo wake uitwao Mshumaa ambao aliuachia rasmi tarehe Novemba 8, 2019 ambapo kupitia mtandao wa youtube, video ya wmbo huo umetazamwa zaidi ya watu 1,315,488 huku ukishika nafasi ya pili kwa kuendelea kufanya vizuri na kutazamwa.