Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Historia ya msanii Alikiba kuanzia mwaka 2005-2019 Bongo Flevani
Share
Notification Show More
Latest News
Habari kubwa Magazetini Kenya leo February 3, 2023
February 3, 2023
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo February 3, 2023
February 3, 2023
Breaking: Sheikh Mkuu DSM atumbuliwa, sakata la Dr Mwaka na mkewe
February 2, 2023
Mason Greenwood afutiwa mashtaka
February 2, 2023
Tanzania Ligi namba 5 kwa Ubora Afrika
February 2, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Habari za Mastaa > Historia ya msanii Alikiba kuanzia mwaka 2005-2019 Bongo Flevani
Habari za Mastaa

Historia ya msanii Alikiba kuanzia mwaka 2005-2019 Bongo Flevani

November 14, 2019
Share
3 Min Read
SHARE

Ni msanii wa Bongo Fleva Alikiba mwenye umri wa miaka 32 ambae headlines zake zilianza mwaka 2005 ambapo kupitia wimbo wa msanii Abby Skillz alijulikana baada ya kushirikishwa katika wimbo uitwao Maria

Safari ya Alikiba ikamuendelea murua ambapo mwaka 2007 aliachia rasmi album yake ya kwanza yenye jina la ‘Cinderella’ yenye nyimbo 15 ambazo zilizopendwa na kukubali.

Ilipofika mwaka 2010 Alikiba alipata shavu kubwa la kuwa miongoni mwa wasanii walioshiriki kuimba wimbo wa Hands Across the World uliyosimamiwa na Staa R Kelly na kusambazwa na Sony Music & Rockstar4000.

Hands Across the World ni wimbo uliokutanisha wasanii 8 kutoka mataifa tofauti Afrika akiwemo, R.Kelly, 2Face, 4×4, Alikiba, Amani, Fally Ipupa, JK, Movaizhaleine & Navio

 

Ukimya wa Alikiba ulianza mwaka 2010 ambapo mkali huyo aliamua kukaa kimya takribani miaka 4 na aliporudi mwaka 2014 kwenye muziki  wa Bongo Fleva aliachia video ya wimbo wake mpya uitwao MWANA.

MWANA ulikuwa ni wimbo wa kwanza uliosimamiwa na lebo ya Rockstar4000 enzi hizo chini ya meneja Seven Mosha, baada ya hapo zikafuata mwendelezo wa hits mbalimbali kali zikiwemo, Seduce Me, Aje, Lupela, Chekecha Cheketua, Kadogo, Mvumo wa Radi na nyinginezo kali

Safari yake ya muziki ikaendelea na ilipofika mwaka 2016 staa huyo alisainiwa na Sony Music ambapo mnamo tarehe 19 mwezi mei Alikiba alifika nchini Afrika Kusini katika ofisi za Sony Music kusainiwa rasmi.

Moja ya kazi za mkataba huo ni kumtengeneza Alikiba kwenye kiwango cha juu zaidi kimuziki, kibiashara na kugharamia video zake na anaporekodi audio zake, kila anapotoa muziki mpya unaachiwa kwa nguvu ya usimamizi wa Sony Music kwenye masoko makubwa ya muziki kama Marekani, Ulaya na Africa.

Unaambiwa mkataba aliokuwa ameusaini Alikiba unafanana na ule aliosaini mwimbaji staa wa Nigeria Davido ambapo una vipengele vya kusababisha collabo kwa urahisi zaidi na mastaa wakubwa wakiwemo wa marekani.

Baada ya kusainiwa na Sony Music tukazishuhudia hits kali na collabo mbalimbali zilizochukua vichwa vya habari

Safari ya Alikiba ikaendelea kupamba moto kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva ambapo mwaka 2018 aliamua kuwatambulisha rasmi wasanii wake anaowasimamia katika lebo yake iitwayo King Music Records

Wasanii hao ni Cheed, K2ga, Killy ambapo single yao ya kwanza ilitambulika kwa jina la Mwambia SINA, Baada ya hapo zikafuata mfululizo wa hits mbalimbali ikiwemo Rhumba, Toto 

Kwasasa Alikiba anazimiliki spika za radio kwa wimbo wake uitwao Mshumaa ambao aliuachia rasmi tarehe Novemba 8, 2019 ambapo kupitia mtandao wa youtube, video ya wmbo huo umetazamwa zaidi ya watu 1,315,488 huku ukishika nafasi ya pili kwa kuendelea kufanya vizuri na kutazamwa.

 

You Might Also Like

Exclusive: Dully Vanny kwa uchungu azungumzia video chafu aliyotajwa, amtaja diamond na mama yake

Audiomack yazindua kampeni ya ‘Ngoma juu ya ngoma’ kukuza muziki wa kitanzania

Exclusive: Con boi kafunguka hana mawasiliano na Lunya,Quick Rocka, akumbuka kifo cha mpenzi wake

Dj Khaled ametuletea hii video mpya ‘Staying alive’ akiwa na Drake na Lil Baby

Mkali Burna boy ametuletea hii video mpya akiwa amemshirikisha Ed Sheeran

TAGGED: alikiba, bongo fleva, One8
Edwin TZA November 14, 2019
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Mkamia amuambia Waziri Mkuu “Tuwe wakweli kuna njaa”, akubali kweli njaa ipo (+video)
Next Article VideoMPYA: Abdukiba katuletea mdundo mpya kamshirikisha G nako
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Habari kubwa Magazetini Kenya leo February 3, 2023
Magazeti February 3, 2023
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo February 3, 2023
Magazeti February 3, 2023
Breaking: Sheikh Mkuu DSM atumbuliwa, sakata la Dr Mwaka na mkewe
Top Stories February 2, 2023
Mason Greenwood afutiwa mashtaka
Sports February 2, 2023

You Might also Like

Sports

Tanzania Ligi namba 5 kwa Ubora Afrika

February 2, 2023
Sports

Mchezaji mwenye umri mkubwa (55) asaini Ureno

February 2, 2023
Sports

PSG wachukizwa na Chelsea kukwamisha usajili wa Ziyech

February 1, 2023
Sports

Enzo avunja rekodi ya Uingereza usajili

February 1, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?