Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Wakili Paul Kaunda dhidi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kwamba amekosea kufungua shauri hilo. Mbali na Ndugai, walalamikiwa wengine ni Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Wakili Paul Kaunda anaiomba Mahakama Kuu kutengua Amri ya Spika Ndugai ya kumtambua Mwambe kama Mbunge halali wa Ndanda Akisoma uamuzi huo Jaji Issa Maige akishirikiana na Jaji Stephen Magoiga na Jaji Seif Kulita alisema mlalamikaji alikosea namna ya kufungua kesi ya kikatiba badala yake alipaswa kufungua kesi kwa utaratibu wa kawaida.
Alisema kuwa kauli ya Spika Ndugai aliyoitoa haikuwa imevunja katiba bali ni ya kiutaratibu katika shughuli zake za kiutendaji hivyo mlalamikaji angekuwa sahihi kama angefungua kesi hiyo kwa utaratibu wa kawaida kwa kutumia Ibara ya 83 (1) badala ya ile ya 26 (2) aliyoitumia.
”TUMUOMBE RAIS WETU, MATAIFA MENGINE YANAKOPI TANZANIA” WAZIRI JAFO