Top Stories

Video:Kesi ya Zitto Kabwe mahakama yapanga kutoa hukumu ‘Tumefunga ushahidi’

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kupanga tarehe ya hukumu katika kesi ya uchochezi inayomkabili mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe baada ya kufungwa kwa ushahidi wa utetezi wa mashahidi 8.

Ushahidi huo umefungwa baada ya shahidi wa nane, Nassib Kapagila kutoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi anbapo Wakili wa utetezi, Jebrah Kambole akaieleza mahakama hiyo kuwa wamefunga ushahidi wao.

Baada ya kueleza hayo Hakimu Shaidi akaamuru pande zote kuwasilisha hoja za mwisho kabla ya Aprili 28 na kesi kurudi tena Aprili 29, 2020 kwa ajili ya kupanga tarehe ya hukumu.

Soma na hizi

Tupia Comments