Top Stories

VIDEO:Maagizo ya Waziri Ummy na Bashungwa kwa wazalishaji wa vifaa vya kujikinga Corona

on

Wamiliki wa viwanda vya Dawa, na vifaa tiba nchini wametakiwa kuanza kuzalisha vifaa kinga kuweza kukabiliana na janga la Corona nchini ili kuondokana na changamoto ya ucheleweshaji wa kupata vifaa kinga toka nje ya nchi pamoja na kupunguza gharama.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na Umoja wa Wazalishaji Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba (TPMA) nchini kwenye mkutano wa kuangalia jinsi gani wanaweza kuzalisha vifaa kinga kutoka wazalishaji wa ndani hapa nchini. “Tukizalisha hapa nchini tutaokoa rasiliamali fedha nyingi, muda pia tutazalisha ajira na kuwa na uhakika wa ubora na usalama unaohitajika kupitia mamlaka zetu za ndani kwa urahisi”. Alisema Waziri Ummy.

Waziri amesema kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa vifaa kinga , hivyo wale wote wanaozalisha vifaa kinga wanatakiwa kuongeza uzalishaji ili kutosheleza mahitaji ya soko nchini na hata kuweza kuuza nchi za jirani. Aidha, amesema Wizara inahitaji kuipa nguvu huduma salama kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya serikali na visivyo vya Serikali kwa watumishi wa afya kuzingatia miongozo ya kukinga na kudhibiti maambukizi angalau kuvaa barakoa,glove na eproni hivyo amewasisitiza kuzalishaji vifaa vyenye viwango vyenye ubora ili kukidhi soko la ndani nan chi za jirani.

Soma na hizi

Tupia Comments