Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Morogoro limebaini kuwepo kwa sehemu isiyo halali ya kuhifadhia mitungi ya gesi katika mtaa wa Bima Manispaa ya Morogoro ambalo lipo karibu na makazi ya watu na kusababisha hofu kwa wakazi wa eneo hilo.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Stephen Katte akizungumza mara baada ya kufanya operasheni katika moja ya nyumba katika mtaa huo na kubaini kuwepo kwa mitungi ya gesi zaidi ya miambili ikiwa imehifadhiwa kinyume na utaratibu.