Top Stories

Video:Mmiliki wa IPTL alivyoondoka Mahakamani Kisutu baada ya kulipa Mil.200

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru kwa masharti Mmiliki wa Kampuni ya Kufua umeme (IPTL), Herbinder Seth, huku pia akitakiwa kulipa fidia ya sh. bilioni 26.9 kwa serikali. Hatua hi iyo imekuja baada ya Seth kuingia makubaliano na DPP ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamkabili kwa njia muafaka.

Aidha Seth amekubali kuweka hati ya kiwanda cha kufua umeme cha IPTL chenye namba 45566 kiwanja namba 292/2 kilichopo Kunduchi Salasala kama dhamana iwapo atashindwa kulipa fedha hizo. Hata hivyo, mshtakiwa Seth ameshalipa kiasi cha sh. Milioni 200 na kiasi kilichobakia anatatakiwa kukilipa ndanj ya miezi kumi na mbili kuanzia leo Juni 16, 2021.

MSHTAKIWA HERBINDER SETH ATOA KAULI MAHAKAMANI “TUKUTANE KWA MKAPA”

 

Soma na hizi

Tupia Comments