Habari za Mastaa

Video:Msemaji wa Serikali amefika kwenye studio za S2kizzy zilizovamiwa DSM

on

Baada ya kuripotiwa kwa taarifa za kuvamiwa kwa studio za mtayarishaji S2kizzy zilizopo Sinza usiku wa kuamkia leo, Sasa Msemaji wa Serikali Dkt Hassan Abbas amefika katika studio hizo na kuongea haya.

Tumesikia hili tukio ambalo limetoka katika studio na mnafahamu kwamba Serikali inatambua shughuli za Sanaa ni shughuli rasmi na tunazitambua na kuziheshimu, sasa tumesikia hilo tukio tumesikitishwa kidogo’- Dkt Hassan Abbas

‘Sheria itachukua mkondo wake maana hapa watu wamepigwa na vitu pia vimevunjwa kwahiyo ishu hii ni ya Polisi ila lazima Sheria ichukue mkondo wake, Sanaa ni kazi rasmi’- Dkt Hassan Abbas

STUDIO ZA PRODUCER S2KZY ZA VAMIWA, WAVULIWA NGUO NA KUPIGWA, HANSTONE AELEZEA ILIVYOKUWA

 

 

Tupia Comments