Top Stories

VIDEO:Rais Magufuli na Rais Kenyatta wameyamaliza sasa ni shwari

on

NI Mei 20, 2020 ambapo Rais Magufuli akiwa safarini kutokea Chato sasa alisimama mkoani Singida kuwasalimia wananchi na kuzungumza machache yakiwemo kuhusu kupigiwa simu na Rais wa Kenya.

‘Juzi nilipigiwa simu na Kenyatta nikiwa bado Chato, akanipa pole na kujielezea mambo ya corona kidogo, leo pia mimezungumza nae pia, kuna kimgogoro kule mpakani mwa Kenya, Kenya ni Marafiki zetu, corona isiwe chanzo cha migogoro, sisi Marais tumeyamaliza’-Rais Magufuli akiwahutubia Wananchi Singida

‘Mimi na Kenyatta tumeongea kwenye simu tumeyamaliza, naagiza ndani ya wiki hii, Waziri wa Uchukuzi na Timu yake wakakutane na Waziri wa Kenya kule mpakani wakiwa na Wakuu wa Mikoa ya mipakani kama Mwanza, Mara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga ili wajadiliane”-JPM

Viongozi wa Mikoa wasitatue matatizo kwa jazba, nafahamu ukichokozwa sana ukanyamaza na wewe unachokoza kidogo sio mbaya, ila tumeyazungumza na Kenyatta tumeyamaliza, Mawaziri na Wakuu wa Mikoa pia mkutane na wenzenu Kenya yaishe haya, ndani ya wiki hii “-JPM

Soma na hizi

Tupia Comments