Top Stories

Video:Wanaodaiwa kumteka Seleman wafikishwa Mahakamani ‘Wametakatisha Mil.30’

on

Watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka manne ikiwemo la utekaji nyara.

Washitakiwa hao ni Angellah Kiwia(41) na mwenzake, Mohamed Rushaka(36) ambao wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Ester Martine, mbele ya Hakimu Mwandamizi, Rashid Chaungu.

Wakili Martine amedai katika shtaka la kwanza, washtakiwa wanadaiwa kati ya Machi mosi na Machi 31, 2020 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, kwa makusudi washtakiwa waliongoza genge la uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.

Katika shtaka la utekaji nyara kwa lengo la kudhuru, washtakiwa wanadaiwa siku hiyo katika jiji la Dar es Salaam, walimteka Seleman Mohamed wakiwa na lengo kumpeleka katika hatari ya kumuumiza. Martine amedia washtakiwa hao wakiwa na lengo la kulipwa walidai kiasi Sh.Mil 30 kutoka kwa Seleman Mohammed, huku wakimtishia kumuua.

Katika shtaka la kutakatisha fedha , washtakiwa hao siku hiyo na maeneo hayo, walijipatia Sh.Mil 30 kutoka kwa Mohamed, huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la makosa tangulizi la kuratibu genge la uhalifu.

Soma na hizi

Tupia Comments