Habari za Mastaa

Kuhusu maandalizi ya video mpya ya wimbo wa Sharomilionea ‘Changanya changanya’

By

on

sharoAliyekua meneja wa Sharomilionea Hemed Kavu ‘HK’ ameongea na millardayo.com na ku-amplify taarifa juu ya video mpya ya wimbo wa Changanya Changanya wa Sharomilionea aliyoshirikishwa Ally Kiba.

Uongozi huo umeipa Exclusive millardayo.com na kuelezea>>’Video tumeifanyia kwa Apex tayari,na kwa sasa tunasubiri vipande vya Allykiba tunasubiri amalize mambo yake tukaingize vipande vyake vya kwenye huo wimbo na baaadhi ya wasanii watakaoshow love kwa Sharomilionea maandalizi  yamekamilika ikiwa ni pamoja na  tshirt zenye sura ya Marehemu Sharomilionea  zipo tayari kwa wale watakaokuwa kwenye video hiyo’

Kuhusu itakavyokuwa kwenye video ukizingatia Mhusika ni marehemu kwa sasa Hk amesema>>’Sharomilionea alishoot verse moja ile ya kwanza na ile ya pili iko nusu haikumaliziwa kuhusu utaalam utakaotumika juu ya vipande vilivyobaki kuna idea 3 ya kwanza ni kuweka mtiririko wa picha zake au kuweka katuni yenye sura yake au kuwatumia watu wanaofanana na marehemu Sharo ambapo kwa hili tutafanya zote kisha tutaangalia ipi nzuri then ndio tuiruhusu’

Hk pia aliulizwa juu ya watu wanaofanana na marehemu Sharomilionea kama kuna waliochaguliwa kwa ajili ya zoezi hilo amesema>>’Mpaka sasa hakuna mtu maalum aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya Marehemu Sharo tutafanya auditon ya kumchagua mtu atakaefaa kuchukua nafasi ya Sharo kwenye hii video hata kama watakua 3 au 4 tutawatumia tu.

 

Tupia Comments