AyoTV

AyoTV: Video ikionyesha fujo za wafuasi wa Chadema kwenye kordo ya Mahakama, kesi ya Zitto na Chadema

on

Screen Shot 2014-01-04 at 1.35.57 AMNi January 3 2014 asubuhi ambapo watu mbalimbali wakiwemo Wafuasi na Wanachama wa Chadema walikua wamekusanyika Mahakama kuu kanda ya 88.5 Dar es salaam wakitaka kujua kitakachotokea manake kesi ya Mbunge Zitto Kabwe dhidi ya chama chake cha Chadema ilikua inaendelea.

Muda mfupi kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo, asubuhi kulitokea fujo baada ya jamaa mmoja alieshtukiwa kwamba anarekodi mazungumzo ya moja kati ya vikundi vilivyokua vimesimama kwenye kordo ya Mahakama kuanza kushambuliwa.

Yani ilikua hivi…….. wakati kesi inasubiriwa kuanza kusikilizwa kulikua na makundi mbalimbali ya hawa Wafuasi, wengine upande wa Chadema, wengine upande wa Mbunge Zitto Kabwe ambapo kwenye hivyo vikundi ndio kuna kimoja kikaanzisha vurumai baada kushtukia mchezo.

Mpaka mwisho, hakikujulikana kilikua kikundi cha upande gani kati ya hizi pande mbili za hii kesi ambayo imeahirishwa mpaka Jumatatu January 6 2014.

Unapenda kupata stori za bongo na kuwa karibu na matukio ya kila aina ambayo unaletewa bure kwenye viganya vyako kupitia millardayo.com ? kuwa mwanachama kwa kujiunga na Millard Ayo kwenye facebook, twitter na instagram.

Tupia Comments