Hivi karibuni Serikali ya Tanzania ilipiga marufuku vifungashio vya pombe aina ya viroba na baadaye kuanza ukaguzi ulioanza March 1 2017 ambapo jumla ya viwanda 16 vya kuzalisha pombe kali, maduka ya jumla 18, maghala manne, baa tatu na kiwanda kimoja cha kuzalisha bidhaa za plastiki ikiwemo vifungashio vya plastiki vya kufungashia pombe kali (viroba) vilikaguliwa.
Leo March 5 2017 Waziri wa mazingira na muungano, January Makamba amezungumza kuhusu matokeo ya ukaguzi huo na amesema jumla ya carton 99,171 za pombe kali zilizofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (viroba) zenye thamani ya Tshs bilioni 10.83zimekamatwa.
VIDEO: Faini utakayopigwa ukikutwa na Pombe za Viroba, Bonyeza play hapa chini kutazama
Unazitaka BREAKING NEWS na stori zote? ungana na mimi Ripota wako wa nguvu Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FBTwitter Instagram YouTUBE.