Top Stories

Vigogo Serikalini wakutwa na dawa za kulevya, kamishna ataja mtandao (Video+)

on

Watu wanane wanashikiliwa kwa tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya Dawa za Kulevya huku miongoni mwa Watuhumiwa wakiwa ni Watumishi wa Serikali, akiwemo Askari Polisi na Maofisa TRA.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya, Gerald Musabila amesema pia kuna Wanandoa ambao nao walikamatwa.

‘Katika matukio yaliyojitokeza mwezi June jumla ya watu wanane walikamatwa kujihusisha na Dawa za Kulevya na miongoni mwa watu waliokamatwa ni watumishi wa Serikali wakiwemo Askari Polisi na Maofisa TRA’– Gerald Musabila

Tupia Comments