Taaasisi ya kutoa tuzo za watu Wabunifu na waliofikia malengo kwenye nyanja mbalimbali duniani Global TED imetoa tuzo kwa vijana 10 wa kiafrika walioweza kufanikiwa kuleta ubunifu na maendeleo kwenye nchi zao.
Tuzo hizi hutolewa kila mwaka Uingereza na kwa mara ya kwanza Washindi watazungumza na vijana wengine katika hafla itakayofanyika Arusha Tanzania August 2017.
Kwa Afrika mashariki Mwanahabari mchunguzi Yasin Kakande kutoka Uganda ameweza kuingia kwenye list hii kwa kufanikiwa kupata habari za kiuchunguzi zinazohusu uvunjifu wa haki za binadamu kwa Wafanyakazi wa kiafrika kwenye nchi za mashariki ya kati (Middle East).
Mwanabailojia aliyegundua tiba ya fangas kwenye mwili wa binadamu Mennat El Ghalidkutoka Egpt amefanikiwa kushinda tuzo hiyo kama kijana aliyeleta mapinduzi kwenye sekta ya tiba na afya pia mtaalam wa computer Abdighani Diriye kutoka Somalia na Mchekeshaji Carl Joshua Ncube kutoka Zimbabwe ni miongoni mwa waliopata tuzo hizo.
VIDEO: Ulipitwa na hii ya Mwanamitindo Mtanzania anayemiliki nyumba New york Marekani?Bonyeza play kutazama