Vijana wawili ambao majina yao hayajafahamika wamechomwa moto wao na pikipiki waliyokuwa wakiitumia katika eneo la Shivaz katika kata ya Kaloleni Mkoani Arusha wakidaiwa kuiba simu
Lilia Shayo amesema vijana hao walikuwa wamemuibia mwananchi mmoja simu na wakati wanakimbia walizuiwa na wananchi nakuanza kuwashambulia
Wiki mbili zilizopita vijana wengine wawili walinusurika kuuawa huku risasi moja ikifyatuliwa hewani baada ya vijana hao kuiba simu jambo lililopelekea wananchi kuichoma moto pikiiki waliyokuwa wanaitumia
Baada ya vijana hao kuchomwa moto walichukuliwa na askari wa jeshi la polisi baada ya wananchi wenye hasira kali kuwachoma moto.