Jumla ya Vijana 200 waliokatisha masomo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo ndoa na mimba za utotoni na changamoto za kifamilia wamepata ufadhili wa kuendelea na masomo kupitia Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ushetu katika Chuo cha Maendeleo Msaginya FDC mkoani Katavi.
Akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga Vijana hao Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe Emmanuel Cherehani amewaasa kuitumia vyema fursa hiyo ikiwemo kusoma kwa bidii na kuwa na nidhamu katika kipindi chote watakapokuwa masomoni.
Katika hatua nyingine Cherehani amesema katika kipindi chote cha utawala wake ameendelea kufadhili masomo ya Wanafunzi mbalimbali wakiwemo wa elimu ya juu.
Kwa upande wake mratibu wa elimu kata ya Nyamilangano ilipofanyika hafla hiyo, Kote Chacha akiwasisitiza kuwa waadilifu huku baadhi ya Wazazi na Wanafunzi hao wakimshukuru Mbunge Cherehani kwa fursa hiyo adhimu.
Hatua hiyo inalenga vijana hao kufikia ndoto zao kupitia fani mbalimbali ambapo kati yao Wasichana ni n150 na Wavulana 50.