Vijana wametakiwa kujitokeza kugombea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika novemba 27 mwaka huu ukitanguliwa na zoezi la kujiandikisha kuanzia octoba 11 hadi 20 mwaka huu.
Wito huo umetolewa na mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mussa Kilakala baada ya kuhitimisha zoezi la mbio za pole zizilolenga kuhamasha wananchi kujitokeza katika zoezi hilo.
DC Kilakala amesema wananchi wote wajitokeze kuanzia zoezi la kujiandikisha hadi kupiga kura huku akisisitiza kuwa Usalama upo wa kutosha Serikali imeimarisha Ulinzi wakutosha.
Naye Afisa uchaguzi Manispaa ya Morogoro Shabani Duru amesema jumla ya mitaa 294 ndiyo itakuwa na vituo vya kujiandikisha na kupiga kura na Watu 283,000 wakitarajiwa kujiandikisha katika zoezi hilo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Morogoro Emanuel Mkongo amesema wamejipanga kutoa hamsa Kwa makundi yote yakiwemo walemavu,wanawake na vijana.
Sophia Kalinga ni mmoja wa wakazi wa Morogoro walioshiriki hamasa hiyo amesema mbinu inayotumiwa na viongozi kuhamasisha wananchi ni nzuri kwani inakutanisha Watu wa rika zote.
Sophia anasema kama kijana watashirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa elimu ya ushiriki wa vijana katika zoezi hilo Ili kundi hilo lisiachwe nyuma kwani ndio chachu ya maendendeleo.