Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Seneti ya Vyuo Vikuu na Vyuo vya kati mkoa wa Iringa wanategemea kuwa na ugeni wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohamed Kawaida ambapo atawasili mkoani Iringa March 14 , 2024 na ataendesha semina ya mafunzo kwa Viongozi wa UVCCM vyuo na Vyuo Vikuu
Akizungumza na waandishi wa Habari katika makao makuu ya Ccm mkoa wa Iringa Akida Mnyamis Akida , katibu Hamasa Uvccm vyuoni Iringa amewataka vijana wa vyuo vikuu kujitokeza kwa wingi na kumpokea kuongozi huyo ambapo pia march 16 , 2024 Kawaida atafanya Mkutano wa vijana wa vyuo vikuu na kati
“Nitoe wito kwa wanannchi wote vijana hasa hasa vijana wa vyuo na vyuo vikuu na siku hiyo kutakuwa na vitu mbalimbali ambapo kutakuwa na semina ya viongozi wa vyuo na vyuo vikuu na tarehe 17 kutakuwa na mkutano mkuu kwaajili ya kuwasikiliza viongozi pamoja na mwenyekiti wa vijana Ccm Taifa “