Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Davidi Kihenzile amewataka vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kukijua chama chao na Nchi yao ili kujibu hoja za baadhi ya watu wanaopotosha shughuli za Serikali kupitia mitandao ya kijamii.
Kihenzile ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na Vijana wa Chama hicho kwenye kikao cha Baraza la UVCCM mkoa wa Dodoma amesema kutokana na vijana hao kutokuja mambo na kufuatilia masuala mbalimbali yanayohusu Nchi ndio inapelekea kushindwa kujibu hoja na kueleza mafanikio ya chama na serikali kwenye mitandao ya kijamii.