Hulda Daudi (25) ni Msichana aliyefeli kidato cha nne na kuja Dar es Salaam kutafuta maisha akitokea Morogoro baada ya Baba yake kufariki na kumuachia mzigo wa kumtunza Mama yake pamoja na Wadogo zake.
Akiwa Dar es salaam aliajiriwa saluni kisha baadaye akapata mtaji wa kufungua saluni yake karibu na alipopanga, Tabata kwa Swai, mzigo wa majukumu ya Kifamilia ukamfanya akope fedha kwa zaidi ya Watu watatu wanaokopesha kwa riba ili akuze mtaji lakini mambo yameenda tofauti na amejikuta na madeni mengi, akaamua kujiunga na VICOBA viwili na kote anadaiwa zaidi ya Tsh. Milioni 3.