Siku chache baada ya kufanyika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji hapa nchini, viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) tawi la Mtambani kata ya Mapinga Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, wamewataka wanachama kutulia wakati viongozi hao wanafanya tathimini ya nini kifanyike, kufuatia aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Uenyekiti kitongoji cha Mtambani kushindwa uchaguzi huo.
Wakiongea kwa nyakati tofauti katika mkutano wa tathimini ya uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji kata ya mapinga bagamoyo mkoani pwani baadhi ya viongozi hao wamesema wapo watu waliohusika kuhujumu chama na kukionesha kuwa kimeshindwa kwa muongozo pamoja na katiba kama watapatikana basi watachukuliwa hatua.
Aidha viongozi hao wamedai kuwa kwa matokeo yaliyotangazwa kuwa si halali katika tawi la Mtambani kata ya Mapinga Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani,na hii ni baada ya chama pinzani CHADEMA kujitangazia ushindi wa kiongozi wao.
Viongozi hao pia wamedai kutaka kukata rufaa ya kupinga matokeo hayo na kutaka uchunguzi ufanyike kwa kina kwani wapo na vithibitisho vyote vya idadi ya kura alizopata mgombea wao ambaye kwa sasa inadaiwa kuwa hajachaguliwa.