Salam za heshima pia zilimiminika Jumatatu kutoka kwa viongozi wengine wa ulimwengu, ambao walituma pongezi kwenye mtandao wa kijamii wa X
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliandika, “Rais Trump huwa na maamuzi, na amani kupitia sera ya nguvu aliyotangaza inatoa fursa ya kuimarisha uongozi wa Marekani na kufikia amani ya muda mrefu na ya haki, ambayo ni kipaumbele cha juu.”
Trump hakutaja waziwazi katika hotuba yake ya vita vinavyoendelea nchini Ukraine, ambavyo Urusi ilivamia mwaka 2022, akisema tu kwamba alitaka kukumbukwa kwa kusimamisha vita.
Mkuu wa NATO Mark Rutte alisema kwenye X kwamba kurudi kwa Trump “kutatoza matumizi ya ulinzi na uzalishaji” katika muungano huo.
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer alichapisha video akituma “pongezi zake za dhati” kwa Trump kwa kuapishwa kwake na kuusifu muungano wa Uingereza na Marekani.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi alimpongeza “rafiki yake mpendwa” Trump, akiandika, “Ninatarajia kufanya kazi kwa karibu kwa mara nyingine tena, ili kufaidisha nchi zetu zote mbili, na kuunda mustakabali bora wa ulimwengu.”
Waziri Mkuu wa Kanada Justin Trudeau alimpongeza rais mpya, akiandika, “Canada na Marekani zina ushirikiano wa kiuchumi uliofanikiwa zaidi duniani. Tuna nafasi ya kufanya kazi pamoja tena – kuunda nafasi zaidi za kazi na ustawi kwa mataifa yetu yote mawili.