Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI) nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inaendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita.
Miongoni mwa misheni nyingi za waangalizi wa uchaguzi zilizotumwa kwa ajili ya mchakato huu, mojawapo ya muhimu zaidi ni ile ya muungano wa Makanisa ya Kikatoliki na Kiprotestanti, inayoitwa Baraza la Kuu la Maaskofu wa makanisa ya Katolika na Kiprotestanti (Cenco ECC). Muungano huo wa makanisa ulitoa hitimisho lake la kwanza Alhamisi, Desemba 28 katika ripoti ya awali.
Baraza la Kuu la Maaskofu wa makanisa ya Katolika na Kiprotestanti (Cenco ECC) limetaja kuwepo kwa ”kasoro nyingi na udanganyifu” katika uchaguzi wa hivi karibuni nchini humo
Pia limetaja makosa ambayo yanaweza kuathiri uadilifu wa matokeo.
Cenco inaiomba CENI kufafanua kama matokeo hayo yanaweza kuathiri mchakato huo. Kulingana na Donatien Nshole, katibu mkuu wa Cenco, hoja nyingi bado zinazua maswali mengi.
Mkuu wa kongamano la maaskofu wa kikatoliki nchini humo Donatien Nshole, amesema ujumbe huo umegundua visa vingi vya ukiukwaji wa taratibu za upigaji kura ambavyo huenda vikaathiri uadilifu wa matokeo ya kura mbalimbali katika maeneo tofauti.