Michezo

Samatta sasa uso kwa uso na Virgil van Dijk

on

Chama cha soka ulaya leo kimechezesha droo ya kupanga makundi ya UEFA Champions League msimu wa 2019/2020, baada ya game za Play off kumalizika.

UEFA wamepanga makundi nane huku mtanzania Mbwana Samatta anayetarajiwa kuwa mtanzania wa kwanza kucheza UEFA Champions League, timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji imepangwa Kundi E na timu za Napoli, Liverpool pamoja na Salzburg.

Kupangwa huko ni wazi sasa Mbwana Samatta anaenda kukutana uso kwa uso na beki bora wa UEFA pamona na mchezaji bora wa Ulaya Virgil van Dijk wa Liverpool baada ya kupangwa Kundi moja.

Makundi 8 ya UEFA Champions League yaliyopangwa leo

Soma na hizi

Tupia Comments